Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni za chama hicho Septemba 28, 2025, mjini Chalinze mkoani Pwani.
Hapa Akizungumza na wakazi na wananchi Chalinze Pwani ambapo amewaomba wananchi hapo kumpigia kura ya ndiyo kwa nafasi ya urais, Wabunge na Madiwani itakapofika Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote.