Katibu Mkuu wa Chama Cua Mapinduzi CCM Dkt. Asha Rose Migiri akimkabidhi kadi ya uanachama Khalfani Bar’wani aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya chama cha CUF na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya kujiunga na CCM katika. mkutano wa kampeni uliohutubiiwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Mgombea Uraia kwa tiketi ya CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
……………
Viongozi wa vyama vya upinzani akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Lindi, Salum Khalfani Bar’wani, wameunga mkono juhudi na utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao kutoka CHADEMA na Chama Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Lindi wameamua kujiunga na CCM wakieleza kuwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya chama hicho umeleta tija kwa Taifa na kuwavutia kujiunga rasmi.
Akizungumza mbele ya Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 25, 2025 kwenye uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi, Khalfani Bar’wani amesema kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kuleta maendeleo ya kweli, hivyo anastahili kuungwa mkono na kila Mtanzania.
Khalfani Bar’wani amewaomba wananchi wa Mkoa wa Lindi kumpigia kura ya “Ndiyo” Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wanachama hao kutoka vyama vya upinzani walikabidhi kadi zao za CHADEMA NA CUF na kukabidhiwa kadi za CCM, huku wakieleza furaha yao kwa kurudi “Nyumbani”.