Mgombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Sabasaba Leo Septemba 26, 2025 kwa ajili ya kuwahutubia na kuwaomba kura za ndiyo wananchi Hao kumpigia kura ifikapo Oktoba 29,2025, katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika nchini kote.
Dkt. Samia ataeleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020/ 2025 na kuwaambia namna watakavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/2030.