Wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan Septemba 23, 2025 wakimsubiri kwa hamu kusikiliza hotuba yake kwenye uwanja wa Soko la Madini mjini Ruangwa ambapo Dkt. Samia ataeleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020/ 2025 na kuwaambia namna watakavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/2030 huku kakiwaomba wananchi Hao kumpigia kura ya ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
WANARUANGWA TAYARI WAKO UWANIANI, DKT. SAMIA KUZUNGUMZA NAO NA KUWAOMBA KURA
