Na Meleka Kulwa – Dodoma
TotalEnergies Tanzania imeendelea kutoa elimu kwa watoto wa Shule ya Msingi Mnadani kuhusu usalama barabarani, tarehe 24 Septemba 2025, ikiwa ni muendelezo wa Programu hio ambayo ni kwa awamu ya nne na kwa mara ya kwanza kwa mkoa wa Dodoma
Bi. Getrude Mpangile, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa kampuni hiyo, amesema kuwa elimu hii inalenga kuwapa watoto uelewa wa sheria za barabarani na mbinu za usalama wanapokuwa safarini kuelekea shuleni au wanaporudi nyumbani.
Aidha, amebainisha kuwa Mwaka huu, shule saba zitashiriki katika programu hii ya elimu ya usalama barabarani, ikiwemo shule moja ya wanafunzi wenye ulemavu, kuhakikisha kila mwanafunzi anashirikishwa.
”Elimu hii inafundishwa kwa njia ya ubunifu, ikiwemo uchoraji, maigizo na uimbaji, kwa kushirikiana na shirika la Nafasi Art Space.” amesema Bi. Getrude Mpangile
Aidha, amebainisha kuwa Mashindano haya huandaliwa ngazi ya taifa, ngazi ya Afrika, na hatimaye ngazi ya kimataifa mjini Paris, Ufaransa.
Kwa upande wake, Felix Mchira, Mratibu wa Nafasi Art Space, amesema sanaa ni njia rahisi ya kufundisha watoto kutokana na alama nyingi barabarani kuwa michoro na picha. Amesema mpango huu umeendelea kufanikishwa kwa mikoa ya Dar es salaam, morogoro, pwani ( Bagamoyo) na Kwa sasa Dodoma
Kwa upande wake,Gesi Janken, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mnadani, , amesema kuwa mpango huu umesaidia kupunguza ajali kwani shule ipo karibu na barabara kuu, na awali kulikuwa na changamoto za usalama.
Kwa upande wake Jasmin Yasin mwanafunzi wa darasa la Sita katika Shule ya Msingi mnadani, amesema kuwa elimu hii imewasaidia kuelewa alama za barabarani na njia salama za kuvuka barabaraamesema,
”Tumepata ujuzi wa kutumia zebra crossing na kuvuka barabara salama.”