Naibu Katibu RAAWU,Simon Mbai akizungumza kwenye semina hiyo jijini Arusha leo.
Naibu Katibu RAAWU,Simon Mbai akizungumza kwenye semina hiyo jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa RAAWU kanda ya mashariki na Mjumbe wa baraza kuu ,Rajab Kufikiri akizungumza na waandish wa habari jijini Arusha
……..
Happy Lazaro, Arusha
WAAJIRI na viongozi wa matawi ya RAAWU nchini wamekutana jijini Arusha kwa malengo ya kutimiza malengo yao ya kazi pamoja na kutoa elimu kwa lengo la kukumbushana wajibu wao.
Akizungumza kwenye semina hiyo inayoendelea jijini Arusha ,Naibu Katibu Mkuu RAAWU,Simon Mbai amesema kuwa ,lengo la semina hiyo ni kutimiza malengo yao ya kazi ambayo wamekuwa wakijipangia kila mwaka ya kutoa elimu kwa wafanyakazi na waajiri inayoshirikisha viongozi wa matawi pamoja na menejimenti kwa ajili ya kukumbushana na kuelekezana maswala mbalimbali yanayohusu kazi tija na ufanisi.
Amesema kuwa, wanakumbushana maswala mbalimbali ambayo yapo nje na ajira na wanakumbushana kuhusu ujasiriamali pamoja na kuelekezana kuhusu matayarisho kabla ya kustaafa na baada ya kustaafu ambapo wamekuwa wakikumbushana pia kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wanachama wao.
Amesema kuwa fursa kama hizi ambazo zimekuwa zikiwakutanisha watu wa mifuko hiyo huwa zinasaidia kupata ufumbuzi wa hizo changamoto ili na wanachama wao sehemu za kazi wanazipitia.
Mbai amefafanua kuwa kwa sasa hivi teknolojia ina maswala mawili kuna faida na kuna athari za teknolojia pia ndio maana hata kwenye semina yao hiyo wamealika wataalamu na wabobezi waliobobea katika maswala yanayoonyesha changamoto zinazotokana na teknolojia na tumeona teknolojia inavyobadilika inaathiri pia jamii ya wafanyakazi.
Kwa upande wake Katibu wa elimu uenezi na uhamasishaji chama cha wafanyakazi RAAWU, Baraka Shekimweri amesema kuwa, semina hiyo imewashirikisha waajiri pamoja na viongozi wa matawi ya RAAWU kote nchini ambapo amesema lengo la semina hiyo ni kubadilisha na kuhamasishana kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo wajibu wa wafanyakazi wenyewe pamoja na waajiri sehemu za kazi na maswala mbalimbali mtambuka kama maswala ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuhimizana kuhusu usawa mahala pa kazi.
“Haya ni maeneo ambayo tunaamini tukiendelea kukumbushana hivi yatamjengea uwezo mfanyakazi kuwa na.utulivu sehemu ya kazi na kujua mipaka yake pamoja na kuiheshimu mipaka hiyo katika eneo lake la kazi ili aweze kutimiza wajibu wake vizuri .”amesema Baraka.
Amesema kuwa jukumu la.chama cha wafanyakazi ni kule umoja eneo la kazi na mafunzo haya wamekuwa wakifanya kwa mwaka mara moja ambayo yanahusisha matawi yote nchini pamoja na waajiri kwa ujumla.
Amesema kuwa chama cha wafanyakazi ni muunganiko baina ya wafanyakazi pamoja na waajiri ambapo wanatengeneza daraja hapo angalau kuweza kuweka mazingira mazuri eneo la kazi pamoja na kumtengenezea mwajiri malengo yake ya taasisi aliyojiwekea yaweze kufkiwa kwa wakati klna ndio maana tunakuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kwa lengo la kukumbushana.
Baraka amesema kuwa watu wana tabia ya kuishi kwa mazoea na hivyo kimsingi ni lazima tuwe na utaratibu wa kukumbushana kupitia vikao na kupitia semina mbalimbali kama hizo kwani wanapomfanyia mtu mafunzo wanamsukuma kile ambacho alichokuwa amefanya kama ni kibaya aidha kwa uzembe au kwa kukosa ujuzi inamwongezea kitu.
“Mafunzo haya yamekuwa yakiwasaidia ndo maana kama mwaka huu jumla ya washiriki 250 kutoka taasisi mbalimbali wameshiriki hadi sasa na mafunzo haya yanaleta tija ndo maana waajiri wanatuunga mkono na kuwaruhusu waje .”amesema Baraka.
“Chama.chetu cha RAAWU sehemu kubwa ya wanachama wanatoka sekta za utafiti na tunajua hiyo ndio sehemu muhimu katika Taifa hivyo tunajitahidi kuwatengenezea mazingira na kuwajenga wawe na utu na uzalendo wa kulipenda Taifa lao.”amesema.
Kwa upande wake mgenirasmi ambaye ni Mwenyekiti wa RAAWU kanda ya mashariki na ni Mjumbe wa baraza kuu ,Rajab Kufikiri amesema kuwa,malengo ya semina hiyo ni kuwajengea uwezo wafanyakazi na waajiri katika mambo mbalimbali yanayohusiana na mambo ya kazi mahala pa kazi kwa maana ya wajibu na haki ya kila mmoja katika eneo la kazi.
Amesema kuwa mada zitakazofundishwa ni pamoja na chimbuko la vyama vya wafanyakazi na faida zake mahala pa kazi,pamoja na mada nyingine ya mabadiliko ya tabia ya nchi jinsi ambavyo yanamwathiri mfanyakazi mmoja na taifa kwa ujumla wake.
“Semina hizi tusihudhurie tu kwa mazoea tupokee mafunzo na tuyatumie na tuwape na wenzetu yale ambayo tumejifunza kwa mustakabali wa taasisi zetu .”amesema.