Miongoni mwa matukio yaliyovuka hisia kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wananchi wenye ulemavu kutoka Masasi walihudhuria mkutano wa Kampeni mjini Masasi huku wakiwa na Bango lao lenye ujumbe unaoeleza kuhamasika kwao kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025, kutokana na umuhimu wa Mikopo ya Asilimia Mbili inayotolewa na Halmashauri mbalimbali kutoka serikalini kuwa imewaokoa hivyo Oktoba wanakwenda kutiki.
Dkt. Samia Suluhu Hassan alipita kuwasalimia na kuzungumza nao machache hakika asilimia mbili imewaokoa.
Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefanyika Masasi mkoani Mtwara tarehe 23 Septemba, 2025.
Sehemu ya wananchi wa Masasi mkoani Mtwara waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 23 Septemba, 2025.