Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola (kulia) akigawa majiko ya nishati safi kwa wafanyakazi wa mkoa huo, iliyofanyika leo Septemba 23, 2025 katika ofisi za TANESCO Mkoa wa Temeke zilizopo Kurasini, Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa kuhamasisha matumizi ya majiko ya nishati safi.
Afisa uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Bi, Lucia Renatus (wa kwanza kulia) akitoa elimu kwa vitendo ya matumizi ya majiko ya nishati safi Kwa wafanyakazi wa mkoa huo.
Picha za matukio mbalimbali
…………..
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke yafanikiwa kuendelea kutoa elimu kwa wafanyakazi 120 na kugawa majiko 42 ya nishati safi ya ruzuku yaliyofika mkoani hapo kwa wafanyakazi wake, ambapo majiko 9 yamechukuliwa kwa pesa taslimu na mengine 33 kwa njia ya utaratibu wa awamu (mkataba).
Zoezi ili likiwa ni sehemu ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya umeme kwa kutumia vifaa vya umeme na wafanyakazi kwa kauli mbiu ya PIKA KWA UMEME, UMEME NI NISHATI NAFUU ZAIDI JIKONI
Akizungumza leo, Septemba 23, 2025, katika ofisi za Mkoa huo zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam, wakati wa kugawa majiko hayo kwa wafanyakazi kwa mfumo wa ruzuku, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola, amesema kuwa jumla ya majiko 42 yote yamenunuliwa na wafanyakazi.
Mhandisi Mashola amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kuhakikisha wafanyakazi wa TANESCO wanakuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya majiko ya nishati safi, sambamba na kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya nishati chafu za kupikia
Afisa uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Bi, Lucia Renatus, ameongeza kuwa, wakati umefika kwa jamii kutumia majiko ya nishati safi ya umeme. Majiko haya huokoa muda jikoni, ni salama kwa matumizi, hulinda afya, hayatoi moshi, yanatunza mazingira, ni safi jikoni na yana gharama nafuu.
Aidha, baadhi ya wafanyakazi waliopokea majiko hayo, akiwemo Bi. Aisa Msumbusi, wameshukuru uongozi wa Shirika kwa kuwapatia fursa hiyo kupitia utaratibu wa mikopo ya majiko janja, kwani majiko hayo yatakuwa msaada mkubwa katika kulinda mazingira na kupunguza muda jikoni.