Mgombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan akisubiriwa kwa hamu na wananchi wa Nakapanya wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Sptemba 23, 2025, ili kuwahutubia katika mkutano wa Kampeni ambapo pia atawaomba kumpigia kura ya ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini Judith Kapinga akisalimiana na baadhi ya wagonbea udiwani Nakapanya Tunduru wakati wananchi hao wakimsibiri Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kumzikiliza atakapowahutubia na kuwaomba kura ya ndiyo ifikapo Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini note.