Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassani Mwameta amezindua Maonesho ya My Tanzania Roadshow katika Mji wa Stuttgart ambapo zaidi ya kampuni 80 za utalii kutoka Tanzania na Ujerumani zinatangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia maonesho hayo.
Maonesho hayo ambayo huandaliwa na Kampuni ya KILIFAIR ni moja ya majukwaa ya kipekee yanayolenga kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii katika soko la Ulaya.
Utalii ni moja ya kipaumbele muhimu cha Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani katika kuendeleza Diplomasia ya Uchumi. Kupitia majukwaa kama hayo, Ubalozi umeyatumia kuhamasisha utalii na kuifanya Ujerumani kuwa moja ya nchi zinazotoa watalii wengi wanaokuja Tanzania kwa mwaka.