Mgombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akimnadi mgombea Udiwani wa chama hicho, kata ya Businde, Makara Said (kushoto) wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo jimboni hapo, mkoani Kigoma, Septemba 23, 2025. Mgombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kata ya Businde jimboni hapo, mkoani Kigoma, Septemba 23, 2025.
Kigoma 23 Septemba 2025
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mikutano ya nyumba kwa nyumba katika Kata ya Businde akiahidi kushughulikia changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa eneo hilo endapo atachaguliwa
Miongoni mwa changamoto zilizojitokeza ni miundombinu duni ya barabara zinazokwamisha maendeleo na kuongeza gharama za usafiri ambapo wananchi hulipa hadi Sh 4000 kwenda mjini Kigoma Elimu duni ambapo Shule ya Sekondari Businde ina walimu sita pekee na haina maabara huku wanafunzi wakichangishwa Sh 6000 kulipa walimu wa kujitolea Shule ya Msingi baadhi ya wanafunzi wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati Migogoro ya ardhi ikiwemo fidia za KISEZ ambazo wananchi hawajalipwa na mvutano na uwanja wa ndege uliochukua maeneo ya makazi bila tathmini ya haki Afya Kituo cha Afya Businde kimeelezwa kuwa na miundombinu mibovu huduma duni na changamoto kubwa kwa akinamama wajawazito Soko wananchi wakilalamikia kufukuzwa mara kwa mara na kuomba maeneo rasmi pamoja na taa katika magenge ya Mwami Ruyagwa Bei ya saruji wakidai inauzwa kwa gharama kubwa licha ya kuzalishwa karibu Kigoma
Mgombea huyo ameahidi kuwa endapo ACT Wazalendo itashinda katika ngazi ya udiwani ubunge na manispaa changamoto hizo zitashughulikiwa kwa kipaumbele hasa miundombinu ya barabara na huduma muhimu za jamii.