Mkurugenzi wa shule ya Tuishime iliyopo eneo la Njiro Naomi Masenge akizungumzia kuhusiana na mahafali hayo.
………..
Happy Lazaro, Arusha
WAZAZI pamoja na walezi wametakiwa kuwapatia watoto wao malezi mazuri katika kipindi hiki wakiwa majumbani na wasiwaachie watoto wakashiriki katika makundi mbalimbali ambayo hayawapi mafunzo mazuri.
Aidha amewataka kuhakikisha maadili mema na malezi mazuri waliyoyapata watoto hao shuleni hapo yanaendelezwa hata wakiwa majumbani.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkurugenzi wa shule ya Tuishime iliyopo eneo la Njiro Naomi Masenge wakati akizungumza kwenye mahafali ya 15 ya darasa la saba ambayo yaliambatana na mahafali ya wanafunzi wa pre unit.
Amesema kuwa ,shule hiyo ni shule inayotoa wanafunzi wazuri sana kielimu na kitabia kwani wanafundisha masomo ya kawaida pamoja na maadili na dini pia na wana uhakika watoto waliohitimu ni watoto ambao wamekamilika katika mambo yote wanayofundisha katika shule yao.
“Tunapenda tuwakabithi wazazi wawapeleke wanafunzi wao katika shule nzuri ambazo zitaendeleza malezi ambayo tuliwalea katika shule yetu .”amesema Masenge.
Aidha amewataka wazazi kupeleka watoto hao katika shule ambazo zitaendeleza taaluma yao ili watoto wasirudi nyuma kimasomo .
“Huwa tunawaandaa kwa vitendo katika masomo yao ambapo pia programu hizo zipo kwenye baadhi ya vipindi huwa tuna vipindi mbalimbali na ni vitu ambavyo watoto wana uzoefu navyo’amesema Masenge .
Masenge ameongeza kuwa, shule hiyo ilikuwa shule ya tatu au ya nne kuanzishwa katika wilaya hiyo kwa shule za mchepuo wa kiingireza hivyo wanawaasa wazazi ambao wamekuja waendelee kuitangaza shule hiyo katika maeneo mbalimbali ili wapate wanafunzi ambao watawaandaa vizuri kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Aidha ameongeza kuwa, shule hiyo ni shule ambayo inatoa wanafunzi wazuri kielimu na kitabia kwa kuwa inafundisha maadili mazuri ya kidini hivyo ni muhimu wazazi wakahakikisha wanapeleka watoto hao katika shule nzuri ambazo zina maadili mazuri .