NA JOHN BUKUKU- SONGEA
Mgombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye viwanja vya Veta Msamala mjini Songea Mkoani Ruvuma kuhutubia wananchi katika mkutano wa Kampeni ambapo atawaomba wananchi Hao kumpigia kura ya ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Songea waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma tarehe 22 Septemba, 2025, Mkutano uliohudhuriwa kwa pamoja na Mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi pamoja na Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.