Na Mwandishi Wetu, Songwe
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira miongoni mwa sababu za Watanzania kymchagua Mgombea urai wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na uwezo wake kutumia juhudi binafsi kuleta maendeleo ya Watanzania.
Aidha, kupitia CCM chini ya Dk. Samia, Watanzania wataendelwa kuwa salama huku fursa za uchumi zikiendelea kufunguka kupitia sekta mbalimbali ukiwemo uwekezaji.
Aliyaeleza hayo alipozungumza na wana CCM katika mji wa Vwawa, wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe alipokuwa akimtafutia kura Dk. Samia na wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
“Tukiwaambia Watanzania tuchagueni la kwanza tutawathibitishia umoja wa Watanzania utalindwa la pili tutawahakikishia amani ya Tanzania inalindwa na tatu maendeleo ya Tanzania yanapatikana. Mambo matatu; umoja.amani na maendeleo ya kudumu maendeleo ya watu ndio ajenda zetu kuu.
“Kwa hiyo tukija hapa ni mwaka wa uchaguzi, tunapokuja tunawaambia Watanzania tuchagueni hatuwaambii watuchague kwa kubabaisha, tunawaambia tuchagueni kwa sababu sisi ni Chama kinachoahidi na kutekeleza, ndiyo sifa yetu. CCM ni Chama kinachoahidi na kutekeleza na hatujazuia vyama vingine,” alieleza.
Alisema CCM inatambua kuwa wananchi wanataka mambo muhimu zikiwemo huduma bora za kijamii pamoja na uchumi imara.
“Jumuiya ya watu wanataka uchumi, uchumi pamoja na kuwa na chakula cha kutosha, uchumi ni pamoja na kuwa na nyumba nzuri unaishi, uchumi ni pamoja na watoto watapata mahali pakusoma, ukiugua unapata hospitali na unaweza kuwa na uwezo wa kiuchumi na ukanunua nguo zako, angalau mambo matano ambayo yanakufanya uishi maisha mazuri.
“Kwa hiyo mama Samia amerudisha uchumi wetu ulikuwa umeporomoka. Shirika la uchumi duniani IMF (Shirika la Fedha la Kimataifa) limesema uchumi wetu umeimarika unaelekea katika ukuaji kama ulivyokuwa kabla ya Corona, ulikuwa asilimia 6.9 na huenda mwakani tukarudi pale pale asilimia saba.
Uchumi umekuwa, amefungua ameleta uwekezaji, ametangaza Tanzania dunia nzima na utalii ni kielelezo binafsi cha juhudi zake binafsi, alicheza filamu ya Royal Tour, dunia nzima sasa ukisema Royal Tour wanamtaja Samia Suluhu Hassan.
Juhudi zake zimefungua utalii ambao awali ulikuwa ni kwa msimu lakini sasa kula siku wanakuja Tanzania kwa sababu ya kazi aliyoifanya Samia ya kuitangaza Tanzania.
Wawekezaji wameongezeka wanaoweka mitaji yao Tanzania lakini hakukomea katika kujenga uchumi bali ameongeza kasi katika kujenga maendeleo ya jamii.