Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Taifa Ali Hapi, akiwasalimia wananchi,wanachama na wagombea Ubunge wa majimbo yote ya Mkoa wa Ruvuma kabla ya kufungua kampeni za Chama hicho katika Mkoa wa Ruvuma zilizofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Rwinga Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma jana,kulia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Namtumbo Juma Zuber Homera(Picha na Muhidin Amri.
Baadhi ya Wagombea Udiwani wa Mkoa wa Ruvuma kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,wakimsikiliza Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho Ali Hapi(hayupo pichani)wakati wa ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi Mkoani Ruvvuma zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Rwinga Wilayani Namtumbo (Picha na Muhidin Amri).
Wagombea Udiwani wa Viti Maalum wa Mkoa wa Ruvuma,wakiomba kura za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulala chini wakati wa ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi zilizofanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Rwinga Wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma(Picha na Muhidin Amri).
Mgombea Ubunge Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Juma Zuber Homera,akiongea na Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa Kampeni za Udiwani,Ubunge na Urais zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Rwinga Wilayani Namtumbo jana(Picha na Muhidin Amri).
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Namtumbo kupitia Chama cha Mapinduzi Juma Zuber Homer kushoto,akimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Mohmed Halfan baada ya kumaliza kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo la Namtumbo jana(Picha na Muhidin Amri)
…………….
Na Mwandishi Wetu, Namtumbo
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Taifa Ali Hapi,amezindua kampeni ya Urais, Wabunge na Madiwani katika Mkoani Ruvuma,huku akitaja mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi,wagombea ubunge,madiwani na wananchi katika viwanja vya Shule ya msingi Rwinga Wilaya ya Namtumbo alisema,katika kipindi cha miaka minne Serikali ya awamu ya sita imewatendea haki wananchi
wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuleta fedha nyingi ambazo zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji,elimu,afya na miundombinu ya barabara.
Alisema,Serikali imetekeleza llani ya Uchaguzi 2020-2025 kwa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa jingo la wagonjwa wan je(OPD)jingo la mionzi,jingo la kusafisha damu na nyumba ya mtumishi.
Alitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa na kukamilika ni pamoja na ujenzi wa Hospitali za Halmashauri ya Wilaya Nyasa,Mbinga,Namtumbo,Madaba,Songea, na ukarabati wa Hospitali kongwe ya Wilaya ya Tunsuru ni miongoni mwa mafaniko makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amewataka wananchi wa Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma,kumuamini na kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan kwani tangu alipoingia madarakani miaka minne iliyopita, ameonyesha kwa vitendo na dhamira ya kuwajali Watanzania.
Alieleza kuwa,Rais Samia ameendelea kuthibitisha kuwa ndiyo Mgombea mwenye uwezo wa kusimamia na kutekeleza mambo yenye manufaa kwa Watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuliko wagombea wa vyama vingine.
Aidha alisema,Rais Samia Suluhu Hassan amehaidi kuwa,iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika siku 100 za kwanza za uongozi wake,atatoa Sh.bilioni 200 kama mikopo kwa makundi ya vijana ili waweze kufanya biashara ambazo zitawaingizia kipato na kujikomboa na umaskini.
Ahadi nyingine za Rais Samia,ni pamoja kutekeleza mpango wa Bima ya afya kwa wote ambapo katika awamu ya kwanza itawahusu watoto,wazee na watu wa wenye kipato duni,kugharamia matibabu kwa watu wanaougua ugonjwa wa kisukari,moyo,figo na magonjwa mengine ambayo matatibu yake yanahitaji gharama kubwa.
“nawaomba sana wananchi wa Namtumbo,msipoteze muda wenu kuwapigia kura wagombea wa upinzania,hakikisheni mnampa kura nyingi Dkt Samia Suluhu Hassan,mgombea Ubunge Juma Homera na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi”alisema Hapi.
Hapi,amewaomba wana Chama wa Chama cha Mapinduzi kuungana pamoja katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kumpigia kura nyingi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Juma Zuber Homera.
“Homera ni mchapakazi Hodari,anayejishusha kwa watu,mnyenyekevu na mwenye mapenzi makubwa kwa watu wa rika tofauti,anajua matatizo ya Namtumbo,kwa hiyo ndiye suluhisho la changamoto zenu”alisema Hapi.
“Mama Rais wetu Samia Suluhu Hassan,tunahitaji kumsaidia katika majukumu yake,lakini tutamsaidia kwa kumchagulia watu wenye sifa ya kuchapakazi akiwemo Homera”alisisitiza Hapi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Namtumbo Juma Homera,amehidi kujenga soko la kisasa kituo cha mabasi ili kuwezesha wananchi wanaotaka kusafiri kupata huduma kwenye eneo zuri na salama,kujenga barabara za lami pamoja na kumaliza changamoto ya majisafi na salama.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Mohamed Halfan alisema,Mkoa wa Ruvuma umejipanga kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba wagombea wake wanapata kura nyingi kwani kati ya kata 173 kata 80 wagombea wa CCM watapita bila kupingwa na kata 73 vyama vya upinzani vimesimamisha wagombea.
Amewaagiza wanachama wa Chama cha Mapinduzi,kuhakikisha katika kata hizo CCM na wagombea wake wanapata kura zaidi ya asilimia 93.
Naye Mbunge aliyemaliza muda wake Vita Kawawa,amekishukuru Chama cha Mapinduzi kumualika kwenye uzinduzi wa kampeni ya Ubunge na wanachama wa Chama hicho kwa kumuamini katika kipindi cha miaka mitano.
Kawawa,amempongeza Homera kwa kupata ushindi mkubwa kwenye mchakato wa kura za maoni,ambapo amewaomba wananchi wa Namtumbo kumpa ushirikiano na kura nyingi tarehe 29 Oktoba mwaka huu.