Na Sophia Kingimali.
Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanajiandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa NIDA ili waweze kupata huduma za mbalimbali nchini lakini lakini pia usajili huo utasaidia kupata utambulisho na kujitambukisha maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo za kijamii.
Wito huo umetolewa leo Septemba 17,2025 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi idara uzalishaji vitambulisho NIDA Edson Guyai wakiwa kilele cha maadhimisha siku ya utambulisho Duniani huku wao wakitumia siku hiyo kuwahudumia watu wenye mahitaji maalum.
Amesema ili kupunguza idadi ya watu katika vituo mbalimbali vya NIDA amewataka wananchi pindi anapotimiza umri wa miaka 18 akajisajili na kupata kitambulisho hicho.
“Nitoe rai kwa wananchi wahakikishe wanajiandikisha na kupata kitambulisho lakini kupunguza idadi ya watu basi ukiona umefikisha tu miaka 18 nenda ukajisajili hii ni muhimu sana kwani kitambulisho hiki kitakutambulisha na kupata huduma mbalimbali za jamii”,Amesema.
Akizungumza kuhusu kuwafikia makundi maalumu amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anatapata kitambulisho hicho hivyo wameiona changamoto kwa watu wenye mahitaji maalum kujitokeza kupata huduma hiyo ikiwemo changamoto mbalimbali za kuifikia huduma hiyo.
“Leo tunahudumia kundi la mahitaji maalumu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho lakani pia NIDA inajukumu la kuhakikisha kila mwananchi anasajiliwa kwani shughuli zote za kijamii na kiuchumi zinahitaji kitambulisho cha NIDA”,Amesema
Aidha ameongeza kuwa tambulisho huo unasaidia kutambua wageni waliopo nchini lakini pia inawakinga na kuwalinda wananchi na kuwa salama wakati wote pia kupata huduma wanazohitaji kwa wakati.
Amesema kauli mbiu’ya Jisajili tukutambue,tukutambulishe’imeenda sambamba sawa na kauli mbiu ya maazimisho hayo ambayo ni ‘kitambulisho changu Mwamvuli wangu’
Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii na Mratibu wa walemavu Halmashauri ya Temeke Restita Bujiku ameishukuru NIDA na kutaka watu wenyemahotaji maalumu kuitumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe.
“Hii kwetu ni fursa kwani watu wenye mahitaji maalum walikuwa hawajitokezi kwa wingi kujisajili hivyo tunashukuru NIDA kwa kuwaon na kutufikia kwenye Halmashauri yetu”,Amesema Bujiku.
Naye,mmoja ya watu hao wenye mahitaji maalumu Mabadi Mlawa amesema zoezi hilo limewasaidia kwani wengi wao walikuwa hawana vitambulisho na kulazimika kupata huduma kwa kutumia vitambulisho vya ndugu na jamaa zao hali ambayo ilikuwa inawanyima usili wa mambo yao binafsi yakiwemo yakifedha.
“Mimi nitoe wito kwa walemavu wenzangu tuitumie fursa hii tujitokeze kujisajili ili tupate vitambulisho vyetu ambavyo vitatusaidia na sisi kupata huduma mbalimbali kwani huduma nyingi za kijamii zinahitaji namba ya NIDA”,Amesema Mlawa.