NA JOHN BUKUKU
Hali ya hamasa na mapenzi ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo kila picha inayopigwa kwenye mikusanyiko ya kampeni inabeba ushahidi wa imani yao kwa chama hicho na mgombea wake wa urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wameonekana wakishika na kuinua vitabu vya Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025/2030, kama alama ya kukubaliana na sera na mipango ya maendeleo ambayo chama hicho kimeiahidi kuitekeleza mara baada ya ushindi wa Oktoba mwaka huu.
Vijana, akinamama, wazee na makundi mbalimbali ya kijamii wamesimama bega kwa bega katika mikutano ya kampeni, wakionesha mshikamano na mshikikano wa kuunga mkono safari ya ushindi wa CCM. Hamasa hiyo inazidi kutafsiriwa kama ishara ya wazi kuwa chama hicho kimejijengea heshima kubwa kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kote nchini.
Kila mkono unaoshika Ilani, ni sauti ya wananchi wanaotamani kuendelea kuona Tanzania ikisonga mbele kimaendeleo chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ni sauti ya matumaini, ni sauti ya mshikamano, na ni sauti ya ushindi unaosubiriwa kwa hamu na ari kubwa ifikapo Oktoba.