Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 15 Septemba 2025, ameshiriki katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Mkoa wa Kusini Pemba.
Katika mkutano huo wa hadhara, Katibu Mkuu alimnadi Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwahimiza wananchi kumuunga mkono ili kuendeleza maendeleo na ustawi wa Zanzibar.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama na serikali, pamoja na mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo kubwa la kampeni.