Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka, Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025. Pamoja na mambo mengine pia Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA KARDINALI RUGAMBWA IKULU NDOGO TABORA
