Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saleh Muhando, amezindua rasmi kampeni zake kwa kuwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya kampeni na kushirikiana naye katika safari ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Muhando aliishukuru Kamati Kuu ya CCM kwa imani waliyoonyesha kwake kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama, huku akiwataka wananchi kuendeleza mshikamano na mshangao mkubwa alioupata katika mapokezi ya kampeni hizo.
Aidha, aliwaahidi wakazi wa Kilindi kuwa atashirikiana nao bega kwa bega kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi, sambamba na kuendeleza jitihada za chama katika kusimamia maendeleo ya wananchi.
Muhando alisema dhamira yake ni kuhakikisha Kilindi inasonga mbele kiuchumi na kijamii, kupitia ushirikiano wa karibu kati yake na wananchi.