Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Uyui katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani Tabora tarehe 11 Septemba, 2025.
Wananchi wa Wilaya ya Uyui wamefurika uwanjani wakisubiri kwa hamasa kuwasili kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 11 Septemba, 2025.
Dkt. Samia anaendelea na ziara za kampeni za uchaguzi mkuu mkoani Tabora akitokea Singida, ambapo leo anatarajia kufanya mikutano katika wilaya za Uyui, Urambo na Kaliua na kunadi sera na ahadi za Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa wananchi wa mkoa huo.
Sehemu ya Wananchi wa Uyui waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora tarehe 11 Septemba, 2025.