Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Asha Rose Migiro,Jana Jumatatu tarehe 8. Septemba 2025, alifika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kukutanana na Sekretareti Ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Dkt Migiro mbali ya kuishukuru Sekretarieti hiyo kwa mapokezi waliyompa pia amewataka kufanya kampeni za kistarabu kwa kuitaja Ilani ya CCM na maendeleo yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Ilani iliyopita pamoja kuendeleza amani na utulivu.
Aidha Katibu Mkuu alihimiza suala la nidhamu na maandili wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi za kila siku kwa kuwatumikia wanachama na wananchi kwa ujumla.