Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mafanikio yanayoelezwa kote alikopita tangu azindue kampeni za CCM kwa Uchaguzi Mkuu yametokana na dhamira ya serikali yake ya kuinua maisha ya Watanzania wa hali ya chini.
Dkt. Samia alitoa kauli hiyo Septemba 06, 2025 alipohutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Kalenga, mkoani Iringa, ulioshirikisha wananchi wa majimbo ya Kalenga na Isimani.
Amesema tangu alipozindua kampeni zake Kawe, Dar es Salaam, Agosti 28 mwaka huu, amekuwa akipokea ushuhuda kuhusu kazi kubwa illyoteketezwa na serikali yake katika kipindi cha miaka minne akiwa madarakani.
Akiwa Kalenga, Dkt… Samia alibainisha kuwa hoja anazojitokeza mara nyingi ni zile zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa vijijini.
“Kuna maneno wanasema ali serikali si ya wanyonge Nami nikawajibu: siongozi wanyonge, hinanngoza Watanzania Nataka ujenge Tanzania tunavoitaka. Umeme umepelekwa vitongojini, mall vanapatikana Vijijini, vituo vya afya na vipimo vya vya kisasa vipo karibu na wananchi, shule bora zimejengwa-nuko ndiko kumjail mnyonge,” alisema
Ameongeza kuwa serikali yake Itaendelea kurekeleza miradi inayogusa wananchi wa chini, kwa kuwa dhamira yake ni kuwanyanyua na kuwajumuisha katika uchumi wa taifa.
Pia alimshukuru Chifu Adam Abdul Sapi Mkwawa II kwa kumpa baraka, akleleza kuwa Wahehe wanajulikana kwa mapambano, hivyo baraka hizo zitamsaidia kuijenga Tanzania yenye uchuni jumuishi.
Aidha, aliwaahidi wananchi wa majimbo ya Kalenga na Isimani barabara za lami, madaraja na mabwawa ya umwagiliaji, huku akibainisha kuwa serikali yake inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali.
Akihitimisha ziara yake mkoani Njombe kabla ya kuingia Iringa, aliongoza mkutano mkubwa wa hadhara mjini Makambako, ambapo alitangaza kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) utaanza kununua mahindi kutoka kwa wakulima wa Nyanda za Juu Kusini.
Dkt. Samia ameahidi pia kuwa, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena, serikali yake itaangalia maeneo mapya ya kiutawala, ikiwamo kuanzisha wilaya mpya na kupandisha hadhi za halmashauri, kulingana na vigezo vilivyowekwa.
Katika mikutano mingine aliyoifanya Kata ya Nyololo (Jimbo la Mufindi Kusini) na Mafinga Mjini, alisisitiza kuwa serikali yake ijayo itaendeleza kasi ya utekelezaji wa miradi, hasa katika sekta ya usafirishaji wa bidhaa na watu, ili kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi.
Vilevile, aliwahimiza wana CCM kuvunja makundi ya ndam ya chama, III kujmanisha mshikamano na kuhakikisha ushindi wa kismoan katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Ziara yake mkoani Iringa inatarajiwa kukamilika kwa mkutano mkubwa wa kampeni utakaofanyika Jumapili Septemba 07,2025 katika Uwanja wa Samora, Iringa Mjini.