Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishangilia ishara ya uzinduzi wa nembo mpya katika ofisi zao zilizopo Njiro jijini Arusha.
Dokta Mfawidhi kituo.cha Afya Themi,Dokta Charles Sululu akizungumza wakati akizindua nembo hiyo jijini Arusha.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo jijini Arusha.
………..
Happy Lazaro, Arusha
Arusha .KAMPUNI ya nishati jua inayoongoza duniani ya Sun King imezindua nembo yao mpya iliyoboreshwa zaidi ambapo hatua hiyo kubwa inayodhihirisha ukuwaji wa kampuni hiyo.
Aidha kupitia uzinduzi wa nembo hiyo mpya, Sun King yenye kauli mbiu ya “Angaza Maisha Yako” itaendelea kutoa huduma bora za kimataifa ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma hizo kwa uhakika na ukaribu zaidi.
“Hii inadhihirika kupitia kampeni yao mpya ya “PATA ZAIDI “ambayo inalenga ,Uokoaji zaidi –Kupitia bidhaa bora na za bei nafuu kutoka Sun King,Utulivu wa akili zaidi kupitia huduma zao bora.”amesema Anish .
Ameongeza kuwa ,kampeni hiyo pia inalenga katika Chaguo zaidi kwa bidhaa zao ndogo za taa hadi bidhaa kubwa za inverter zenye uwezo mkubwa pamoja na Nishati ya kuaminika zaidi kwa nyumba, biashara na taasisi.
“Nembo yetu iliyoboreshwa inaonyesha dhamira yetu kwa wateja wetu kuendelea kutoa huduma za sola za bei nafuu majumbani na kwenye biashara, vifaa zaidi vinavyorahisisha maisha, na nguvu zaidi ya kukuza biashara, shule na jamii kwa ujumla,
Mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo ya Sun King Anish Thakkar, amesema kuwa Safari ya maboresho ya chapa yetu ya Sun King ni sehemu moja tu ya mageuzi mapana, na wana bidhaa kabambe zinazoguza maisha ya kawaida ya Watanzania zikiwemo,Mifumo ya jua ya HomePlus na HomePlus Pro ambayo hutoa mwanga wa kuaminika kwa kaya pamoja na kuchaji simu.
“SunKing imefunga sola zake kwa kaya zaidi ya milioni 24 huku zaidi ya kaya 300,000 mpya zikiunganishwa kila mwezi barani Afrika.”amesema Anish
Anish amefafanua kuwa ,bidhaa kubwa za sola ziitwazo “inverter system” mbadala wa jenereta zinazopunguza matumizi ya umeme au mafuta hadi asilimia 80 pamoja na simu mahiri za kijanja ambazo wateja wanaweza kulipia taratibu kwa malipo ya awamu.
Amefafanua kuwa, kampuni hiyo ina uzoefu wa kutosha katika sekta hiyo ya nishati ya jua ambapo kwa mara ya kwanza kabisa kumhudumia.mteja wa kwanza ilikuwa mwaka 2009 na hatimaye kuanzia hapo kampuni hiyo ikawa chachu ya kubadili maisha ya watu wengi duniani.
Anish amefafanua kuwa, wameendelea kuwa kutoa suluhisho endelevu kwa mamilioni ya watu ambapo hadi kufikia sasa wapo katika zaidi ya nchi 65 duniani.
“Ikumbukwe kuwa watu takribani bilioni 1.8 duniani wanaishi bila nishati ya uhakika ,na kati ya hao kuna watanzania takribani milioni 13 ambao ni sawa na asilimia 22 ya watanzania wote ,sisi SunKing hatuwezi kukubali hali hii kuwa ni ya kawaida ,hivyo tunafanya kila jitihada kuhakikisha kila mwenye uhitaji anapata bidhaa zetu ambazo zimetengezwa kwa ubunifu na ubora wa hali ya juu.”amesema Anish.
“Tunapokwenda kusherehekea hatua hii muhimu ya uzinduzi wa chapa mpya ya SunKing ifahamike kuwa nembo yetu iliyoboreshwa inaonyesha dhamira yetu kwa wateja wetu kuendelea kutoa huduma za sola za bei nafuu majumbani na kwenye biashara, vifaa zaidi vinavyorahisisha maisha ,na nguvu zaidi ya kukuza biashara.
Katika uzinduzi huu wa chapa hii mpya iliyoboreshwa,Sun King inaendelea kusimamia dhamira yake ya kuangaza maisha ya Watanzania sasa na katika siku zijazo.
Kwa upande wake mgenirami katika uzinduzi huo Dokta Mfawidhi kituo.cha Afya Themi,Dokta Charles Sululu ,amesema kuwa, kampuni ya Sun King ni ya kimataifa inayotoa huduma za nishati jua ambayo imewekeza nchini ikiwa imedhamiria kufikisha nishati ya umeme wa jua kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa gridi ya taifa na sehemu zenye umeme wa gridi ya taifa ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi sambamba na maendeleo ya wananchi.
“Nimefurahi kusikia kuwa kampuni kupitia sera yake ya uwajibikaji kwa jamii imeendelea kutoa misaada ya mitambo ya nishati ya umeme kwenye taasisi tofauti vikiwemo kwenye vituo vya aafya”amesema.
Ameongeza kuwa ,Kituo cha Afya cha Themi ni moja wapo ya wanufaika wakubwa wa juhudi hizo ambapo waliwapatiwa mtambo wa umeme jua ambapo tangu wamepata msaada wa bidhaa yao ya Solar inverter kumekuwa na ahueni mkubwa katika utoaji huduma za afya kwa mama na mtoto na wananchi wa Arusha kwa ujumla.
Dokta Sululu amesema kuwa , kupitia uwekezaji huo wananchi mbali mbali watanufaika kupata bidhaa za nishati jua kwa gharama nafuu pamoja na kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
“Nimesikia kuwa moja ya agenda ya mradi huu ni kufanikisha utunzaji wa mazingira kupitia kuhimiza matumizi ya nishati safi na salama.ambapo aliwahimiza kuendelea na uwekezaji huo wa kuwezesha wananchi kujiletea maendeleo,kama ambavyo wengi wetu mnajua sehemu ikiwa na umeme,maisha ya wananchi yanakuwa bora kuliko maeneo yasiyo na umeme.
“Niwaombe pia kuendelea na jitihada za kushirikiana na vituo vya afya mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa mitambo yenu inaendelea kutumika katika kuchangia uboreshaji wa afya ya mama na mtoto”