“Nimefurahi na nimevutiwa sana na mada ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, ambayo imesheheni mafunzo kuhusu uzuiaji rushwa na maadili, sambamba na Kongamano letu la Uzinduzi wa Kampeni ya Kurudisha Maadili kwa Jamii kuelekea kumbukizi ya mazazi ya Mtume Mohammed (S.A.W).
Ninasisitiza wote tuungane, tukatoe mafunzo na kuyaishi maadili yaliyowasilishwa hapa,”* amesema Dkt. Saleh Mohamed Abdallah wa Idara ya Elimu ya Mahakama ya Kadhi, BAKWATA.
Dkt. Saleh alitoa kauli hiyo baada ya wasilisho la Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Bw. Ramadhani Ndwatah, katika Kongamano la Uzinduzi wa Kampeni ya Kurudisha Maadili kwa Jamii kuelekea kumbukizi ya mazazi ya Mtume Mohammed (S.A.W) lililofanyika Wilayani Korogwe.