Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapindizi (CCM). Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amesema Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan, endapo kama Itaingia Madarakani kwa mara nyingine itahakikisha inatenga maeneo mengine ya kutosha kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo, ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha Utafiti kwenye maeneo ya Madini kutoka asilimia 16 hadi asilimia 50.
Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 05, 2025 akiwa mkoani Geita katika Wilaya za Mbogwe na Nyang’hwale, ikiwa ni muendelezo wa Mikutano ya Kampeni za Urais Kupitia CCM kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.
“Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2025/2030 imedhamiria kuongeza tija kwenye Sekta ya Madini, kwa kutenga maeneo ya Wachimbaji madini wadogo, vile vile Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan inakusudia pia kuongeza kiwango cha Utafiti wa Madini kutoka asilimia 16 hadi kufikia asilimia 50” amesema Dkt Nchimbi.
Dkt Emmanuel John Nchimbi nil Mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, wakipeperusha Bendera ya CCM.