Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia wananchi wa Kisesa na Nyanguge wilayani Magu leo Jumamosi Agosti 30,2025 wakati akielekea mkoani Mara kuendelea na kampeni zake eneo la kanda ya Ziwa ikiwa ni baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Kiswaga Destery Boniventura pamoja na Wagombea Udiwani .