Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Mara,akianza kwa kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini leo Jumamosi Agosti 30,2025 mkoani humo kuendelea na kampeni zake mara baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza.
Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini,Balozi Dkt.Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia aliwanadi Wagombea wa Mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Bunda mjini, Easter Bulaya pamoja na Wagombea wa Udiwani .
Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi yupo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya Kufanya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.