Na Meleka Kulwa -Dodoma
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kufuatilia kampeni pamoja na sera za wagombea wa vyama vya siasa, ili kujihakikishia wanapata viongozi bora na wenye uwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi
Jawadu Mohamed ameyasema hayo Agosti 29,2025 alipokuwa akifanya ziala ya ukaguzi wa eneo la Tambukareli Kata ya Tambukareli liliopo Jijini Dodoma utakapofanyika uzinduzi wa kampeni za ccm mkoa ambapo mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassa anatarajiwa kuzungumzia na wananchi,
Uzinduzi wa Kampeni hizo kwa Mkoa wa Dodoma unatarajiwa kufanyika Agosti 31,2025 ambapo utatanguliwa na Mkutano mwingine wa Kampeni utakaofanyika Kibaigwa Mkoa wa Dodoma Agosti 30,2025
Aidha, Jawadu Mohamed amesema kuwa, Uzinduzi wa kampeni hizo utakuwa wa kihistoria ndani ya Mkoa wa Dodoma
Aidha, amewataka Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Watanzania wote kujitikeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea na kumchagua yule anayemuona anafaa kumwakilisha kama kiongozi mkuu katika eneo analoishi, ili aweze kushughulikia na kutatua changamoto zao
Kwa upande wake Katibu mwenezi wa kata ya Tambukareli Martha Simba amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo unaotarajiwa kufanyika agost 31 yanaendelea vizuri huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi
Chama Cha Mapinduzi kinaendelea na Ratiba za Kampeni, Baada ya Ufunguzi kufanyika Agosti 28, 2025 katika Viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe Jijini Dar es salaam, kuelekea Uchaguzi Mkuu Unaotarajiwa kufanyika hapo baadae Oktoba 29, 2025.