Na. Mwandishi wetu,
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini inasema inasubiri kupokea amri ya mahakama inayotajwa kuzuia uamuzi wa ofisi hiyo kwa muda na kutoa Kibali (leave) kuwaruhusu bodi ya wadhamini ya CHADEMA kuomba judicial review kuhusiana na uamuzi wa msajili kuzuia ruzuku na kutengua uteuzi wa baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa kutokufuata taratibu halali za chama chao
“Nasisi tumesikia kama mlivyosikia nyinyi na kuona mitandaoni, kwa kawaida ofisi yetu inaheshimu maamuzi ya mahakama. Lakini tunayasubiri yatufukie kwa mujibu wa sheria na taratibu za kimahakama za ku sarve hukumu na taarifa zote za kimahakama kutumia ‘Court Process Server’ “. Amenukuliwa Msajili Jaji Fransis Mutungi
Ameongeza kuwa wao hawawezi kushindana na propaganda za kisiasa kutaka kuuaminisha umma kuhusu jambo fulani hata kama halijawa hivyo linavyoelezwa lakini kwa kuwa ni suala linasemwa kutokea mahakamani basi wanasubiri wapatiwe uamuzi rasmi wa kimahakama kama taratibu zinavyotaka
“Bado hatujapatiwa nakala ya amri inayotajwa, na kwa msingi huo hakuna kilichobadilika mpaka hapo tutakapopokea drawn order ya mahakama kuhusiana na shauri tajwa, ikifika hapo taratibu zote za kisheria zitafuatwa”. Ameongeza jaji Mutungi
Jana katika mitandao ya kijamii zimesambazwa taarifa na viongozi na wanachama wa CHADEMA kuwa Mahakama kuu nchini masijala ya Manyara imetoa kibali cha bodi ya wadhamini wa chama hicho kuomba marejeo ya kimahakama kuhusiana na maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa kukubaliana na hoja zilizoletwa kwake na mwanachama wa CHADEMA rembris mchome aliyepinga upatikanaji wa viongozi kadhaa wa chama hicho.