Mgombea Ubunge wa Jimbo la Handeni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saleh Muhando, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Muhando aliishukuru Kamati Kuu ya CCM kwa imani waliyoonyesha kwake kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama katika jimbo hilo.
Aidha, aliwataka wananchi wa Handeni kujitokeza kwa wingi katika kampeni zitakazoanza hivi karibuni, akiahidi kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo endelevu.
Muhando alisema kuwa anakwenda kuendeleza jitihada za chama katika kusimamia maendeleo ya wananchi na kusikiliza changamoto zao ili kuhakikisha Handeni inasonga mbele kiuchumi na kijamii.