Na Mwandishi wetu, Mbulu
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mkoani Manyara, kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mwalimu Stephen J. Siasi, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa nafasi ya Ubunge katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Mwalimu Siasi amekabidhi fomu kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbulu Vijijini Joseph Sambo.
Amewaahidi wana Mbulu vijijini kuwatumikia vyema pindi wakimpa ridhaa ya kuwa mbunge wao.
Amesema yeye ni mchapakazi mahiri hivyo wana Mbulu watarajie mambo mazuri pindi wakimpa ridhaa ya kuongoza.
Mkazi wa kijiji cha Dongobesh, Daniel Tluway amesema wagombea wa jimbo hilo wakiwa wengi ndiyo vyema kwani watasikiliza sera na kubaini mtu wanayemtaka.
“Tumeona CCM na ACT Wazalendo, wamesimamisha wagombea na sasa CHAUMMA wamepeperusha bendera tunatarajia mchuano mkali,” amesema Tluway.