Katibu wa Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, akiongozana na MNEC wa CCM Richard Kasesela wakati alipokagua maadalizi ya uzinduzi wa kampeni za CCM kesho keenye viwanja vya Tanganyika Pakers ambapo Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi na Meenyemiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja Mgonbea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi watatambulishwa na hutubia wananchi.
PICHA NA JOHN BUKUKU- KAWE
……………,.
Na Sophia Kingimali
Katibu wa Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, ametoa wito kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho ili kusikiliza sera na Ilani ya CCM.
Akizungumza leo, Agosti 27, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, alipoenda kukagua maandalizi ya uzinduzi huo, Kihongosi alisema CCM imejipanga kufanya kampeni za kistaarabu bila kutweza utu wa mtu.
Amesema wagombea walioteuliwa na CCM wamebeba matarajio makubwa ya wananchi, na kupitia kampeni hizo watapata nafasi ya kuwaeleza Watanzania yale yaliyotekelezwa na chama hicho pamoja na mipango iliyopo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Wagombea waliochaguliwa na Chama Cha Mapinduzi wanasifa zote za kuwa viongozi. CV zao zimejitosheleza, na pia wamebeba matumaini makubwa ya wananchi wa Tanzania,” alisema.
Kihongosi aliongeza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM imebeba mambo makubwa na matumaini, huku ikitoa majibu kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Aidha, aliwaomba na kuvialika vyama vingine vya siasa kufika katika uzinduzi huo ili kusikiliza sera na Ilani ya CCM, akisisitiza kuwa chama hicho kitatumia jukwaa hilo kueleza sera zake na kuwanadi wagombea wake wa kata na majimbo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam