Balozi wa Tanzania nchini Singapore mwenye makazi yake nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele amewasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Singapore Bw. Harold Lee.
Baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Wizira ya Mambo ya Nje jijini Singapore Mhe. Tembele alifanya mazungumzo na Bw. Lee. Kuhusu masuala ya mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Singapore hasa katika sekta ya biashara, elimu na teknolojia.