Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge tuzo ya mshindi wa kwanza katika uboreshaji wa utoaji huduma. Tuzo hiyo imetolewa leo katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kinachofanyia kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kilichopo jijini Arusha. (Picha na Anton Siame )