Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua aliyekuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda kugombea kiti cha Ubunge kwa Jimbo la Arusha Mjini katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Makonda alikuwa akisubiri uteuzi huo pamoja na wanaCCM wengine sita, ambao ni Ally Said Babu, Hussein Omarhajji Gonga, Aminatha Salash Toure, Mustapha Said Nassoro, Lwembo Mkwavi Mghweno na Jasper Augustino Kishumbua.