Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenan Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mafunzo ya chama kuanzia leo Agosti 23, 2025.
Kihongosi, anachukua nafasi hiyo muhimu yenye dhamana ya kusimamia uenezi wa sera, itikadi na mawasiliano ya chama kwa umma.