Na Meleka Kulwa -Dodoma
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla amesema uteuzi huo umefanywa na vikao vya maamuzi vilivyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , akizungumza na waandishi wa habari Agosti 23,2025 katika Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, wakati akisoma orodha ya makada waliopitishwa kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 baada ya mchujo uliofanywa na vikao vya juu vya chama hicho.
Wagombea waliopitishwa na chama ni Paul Makonda katika Jimbo la Arusha Mjini, Nape Nnauye Mtama, Kangi Lugola Mwibala, Livingston Lusinde Mvumi na Isaya Moses ambaye anachukua nafasi ya Hayati Job Ndugai katika Jimbo la Kongwa.
Makalla amesema baadhi ya waliokuwa wakiongoza kwenye kura za maoni lakini majina yao hayakurudishwa ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu na Samuel Malecela ambaye aliongoza kura za maoni katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Jimbo la Kigoma Mjini, chama kimempitisha Clinton Revocutus maarufu kama Baba Leo licha ya kutoshinda katika kura za maoni.
Aidha,Ester Matiko katika Jimbo la Tarime Mjini, Ester Bulaya Bunda Mjini, Magreth Sitta Urambo na Exaud Kigahe aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara hao wote wamepenya licha ya kutoshinda kura za maoni.
Aidha Kenani Kihongosi ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na CPA Amos Makalla ambaye baada ya mkutano na waandishi wa Habari alitangazwa kuteuliwa kuwa Mkuu Wa Mkoa wa Arusha, akichuka Nafasi ya Kenani kihongosi ambaye ameteuliwa kuwa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndani ya CCM.
Pia, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Balozi Dk Asha-Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wa CCM akichukua nafasi ya Balozi Dk Emmanuel Nchimbi ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi wa 2025