Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkurugenzi wa kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), Davidi Kafulila amefafanua utofauti kati ya Usafiri Dar es salaam Rapid Transit (UDART) na Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es salaam (DART).
Amesema UDART ni shirika la Serikali ambalo linanunua mabasi na kuyaendesha yenyewe na haimuiti mwekezaji kuendesha mabasi iliyoyanunua,lakini DART ni mliki wa miundombinu ya barabara yeye ndio anaalika wawekezaji walete mabasi.
“Kwa hapa Dar es salaam tunaenda kuwa na mabasi ambayo yanamilikiwa na shirika la Serikali UDART na yataendeshwa na shirika hilo na tunakwenda kuwa na mabasi ambayo yataletwa na kampuni binafsi na kuendeshwa na kampuni hiyo binafsi katika utaratibu wa ubia”, amesema Kafulila.
Aidha, ameongeza kuwa mabasi yanayoendeshwa na UDART hayana mwekezaji wa ubia lakini haya mabasi yatakayoletwa kwa mkataba kati ya DART na mwekezaji mwingine ndiyo yatakayoendeshwa kwa utaratibu wa ubia.
“Sasa hivi tayari kunamwekezaji ameshaleta mabasi zaidi ya 90 na muda si mrefu yataanza kutembea kwaajili ya kupunguza msongamano “,