Katibu mwenezi wa ACT WAZALENDO mkoa wa Dar es Salaam na naibu waziri kivuli wa utamaduni sanaa na michezo Monalisa Joseph Ndala amemwandikia barua katibu mkuu wa chama hicho akipinga mchakato uliomteua mgombea urais wa chama hicho Luhaga mpina
Katika barua yake hiyo ambayo pia amewanakili Msajili wa vyama vya siasa na mkurugenzi wa tume huru ya uchaguzi (INEC) ameelezea namba vifungu namba 16 (4), (i),(iii) na (iv) vinavyomzuia kuwa mgombea wa chama hicho
Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo pia mwandishi wetu ameiona inasema kuwa ili mgombea Urais wa ACT WAZALENDO ateuliwe na chama hicho, anatakiwa awe mwanachama wa chama hicho kwa siku 30 kabla ya kuteuliwa kwake kifungu ambacho Mpina kinamkataa
“Nimewasilisha rasmi barua kwa katibu mkuu wangu, nimewanakili pia msajili wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi ili waelewe kinachoendelea ndani ya chama chetu”. Amesema monalisa
Ameongeza kuwa yeye ni mwanachama wa chama hicho tangu kinaanzishwa nakwamba hayupo tayari kukiona chama hicho kikipoteza mwelekeo kwa kukiuka kanuni za uendeshaji wa chama chao kama inavuoelezwa katika kanuni za uendeshaji wa chama za mwaka 2015 na marejeo yake ya mwaka 2024.
Tunaendelea kuwatafuta wahusika wengine wa pande zote kujua msimamo wao juu ya jambo hilo