Msafara wa Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan umelitikisa jiji ma Dodoma baada ya umati mkubwa kijitokeza barabarani katika maeneo yote ambayo msafara huo ulipitia Mara baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo na kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025.
Vifijo na Nderemo vilisikika kila mahali huku vijana wa hamasa kutoka Umoja wa Vijana UVCCM na Chipukizi wakihanikiza na kumshangilia kwa mbwembwe mgombea huyo wa urais mpaka makao makuu wa Chama cha Mapinduzi CCM maarufu kama White House jijini Dodoma ambapo alisalimiana na wana CCM waliojitokeza na viongozi mbalimbali wa CCM na watia Nia ya nafasi mbalimbali zikiwemo ubunge na udiwani.