Mwamvua Mwinyi, Pwani
Katika zoezi la kupiga kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa ubunge wa majimbo tisa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, ameongoza kwa kupata kura za ndiyo 12,074 kati ya kura 12,245 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo rasmi, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM mkoa wa Pwani, David Mramba, amesema Jimbo la Bagamoyo, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoani Pwani, CPA Subira Mgalu, ameongoza kwa kupata kura 3,544 kati ya kura halali 5,335 ambapo jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 5,567, huku 232 zikiwa zimeharibika.
Katika Jimbo la Kisarawe, aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Suleiman Jafo, ameongoza kwa kupata kura 4,412, sawa na asilimia 76 dhidi ya wagombea wengine wanne.
Kwa upande wa Kibaha Mjini, Silvestery Koka ameongoza kwa kura 2,824 ,Jimbo la Rufiji, Muhammed Mchengerwa ameongoza kwa kupata kura 8,465 na Jimbo la Mafia, Omary Kipanga ameibuka kidedea kwa kupata kura 1,186, huku katika Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa ameshinda kwa kura 3,247, sawa na asilimia 62.12.
Mramba ameeleza Jimbo la Kibiti, Amina Mkumba ameibuka kidedea kwa kura 4,712 dhidi ya wagombea wengine wawili.
Mramba anasema jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ameshinda kwa kupata kura8,490.