Mkuu wa Idara ya Wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania PLC Rahma Dachi ( wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya shukrani kwa wasaidizi wa wachezaji wakiwakilishwa na afisa utawala wa Lugalo Golf Club Major Chadiel Msechu ( wa kwanza kushoto). Tukio hilo limefanyika jana wakati wa ugawaji wa tuzo na zawadi kwa washindi wa mchezo wa golf jijini Dar es salaam.
…………
Vodacom Tanzania, kupitia kitengo cha Vodacom Business kinachoshughulika na wafanyabiashara wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa michezo, wamekabidhi tuzo na zawadi kwa washindi tofauti wa mashindano ya golf yaliyofanyika katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Agosti mwaka huu.
Hafla hiyo ilikuwa sehemu ya mashindano ya Vodacom Corporate Masters, yaliyolenga kuhamasisha ushiriki wa wadau kutoka sekta mbalimbali kupitia michezo ya kijamii kama golf.
Tuzo hizo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa kike na wa kiume, wanawake, wanaume pamoja na wachezaji wa golf waliobobea kutoka mashirika tofauti. Kupitia tukio hili, Vodacom iliendeleza dhamira yake ya kuunga mkono michezo, kukuza vipaji na kudumisha uhusiano wa kijamii na wadau wake wa karibu.