Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bi. Amina Juma alipotembelea banda la TRC katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Akihojiwa na TRC Reli TV, Dkt. Chang’a amesema kuwa ameandika waraka unaowataka watumishi wa TMA kutumia usafiri wa treni ya SGR katika safari za kikazi kati ya Dar es Salaam na Dodoma kwa lengo la kuunga mkono uwekezaji wa serikali.
Dkt. Chang’a ameongeza kuwa TMA inafanya kazi kwa karibu na TRC katika kuhakikisha shughuli za ujenzi wa reli na usafirishaji zinafanikiwa katika vipindi vyote vya mwaka kwa kutumia taarifa sahihi za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka hiyo