NA DENIS MLOWE, IRINGA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Taifa CCM, Salim Abri Asas amejitokeza katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugalo kupiga kura kwa watia nia ya ubunge na udiwani katika chaguzi za kura za maoni ya chama hicho inayofanyika nchi nzima leo.
Salim Abri ambaye pia ni mjumbe wa Halmashuri kuu ya Taifa Mkoa Wa Iringa amepiga kura ya maoni majira ya saa sita mchana leo na kisha kuelekea katika shughuli nyingine za kitaifa.
Licha ya kujitokeza kwa MCC Salim Abri wajumbe wengi wamejitokeza katika uchaguzi huo uliofanyika kwa amani na utulivu.
Naye mtia nia katika uchaguzi huo nafasi ya ubunge aliyejizoelea umaarufu kwa hoja zake fupi Islamu Huwel amejitokeza kupiga kura ya maoni katika kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa.
Akizungumza kama ilivvyoada kwa ufupi Islamu alisema kuwa anatarajia kuibuka mshindi katika kura ubunge na kuwa mwakilishi wa jimbo la Iringa mjini katika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.
Chaguzi za kura za maoni za watia nia ya nafasi za ubunge na udiwani ndani ya chama cha Mapinduzi zinaendelea nchi nzima huku kila wagombea wakiamini wataibuka na ushindi kutokana na ahadi mbalimbali walizotoa kwa wajumbe.
Ni jambo la kusubiri na kusikia nani ataibuka kidedea katika kura za maoni na mshindi atasubiri maamuzi ya kamati kuu ya chama kuweza kupitishwa katika eneo husika.