Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Agosti 4, 2025
Katika zoezi la kupiga kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), jumla ya wajumbe 5,743 walijitokeza kupiga kura kati ya 6,300 waliotarajiwa kushiriki.
Kati ya kura hizo, kura halali zilikuwa 5,682 huku kura 53 zikiripotiwa kuharibika.
Katika matokeo yaliyotangazwa rasmi na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Kibaha Mjini, Issack Kalleiya, alisema wagombea walikuwa sita wakichuana kuwania tiketi ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
“Aliyeongoza ni Silvestry Koka aliyekusanya kura 2,824, akifuatiwa na Mussa Mansour (Dangote) aliyepata kura 1,775.”
Kalleiya alitaja wagombea wengine kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Abubakar Allawi aliyepata kura 727, Dkt. Charles Mwamwaja(PHD) kura 282,advocate Magreth Mwihava kura 39, na Ibrahim Mkwiru aliyepata kura 35.
Mchakato huu umefuata taratibu za ndani ya chama, na matokeo haya yatawasilishwa kwa ngazi ya mkoa kisha ngazi za juu kwa hatua na taratibu zaidi za kichama.