Kikundi cha wa ufaika wa Mfuko wa Maendeeo ya Jamii – TASAF katika Manisapaa ya Ilemela mkoani Mwanza nimehakikishiwa kupata ruzuku ya ziada ili kununua mashine ya kusigina karanga.
Uhuru Group, kikundi kinachojishughulisha na usindikaji wa karanga kwa ajili ya matumizi ya kuungia hckuala na kupata kwenye mkate (peanut butter) kimetembelewa na Menejimenti ya TASAF waliotaka kujionea maendeeo ya miradi mbalimbali ya TASAF mkoani Mwanza.
Walengwa hao, mwa msaada wa TASAF na Manispaa ya Ilemela wanatengeneza sabuni za maji na karana zilizosindikwa ambazo huziuza kwa wateja mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF, Shadrack Mziray alijionea jinsi akina mama hao wanavyosigina karanga kwa mikono na utumia Zaidi ya saa 12 kupata karanga zinazotosha kwa uzalishaji wa siku moja.
Wanakikundi hao walimweleza Mziray kuwa wanaoomba msaada wa mashine inayoweza kufanya kazi hiyo kwa chini ya saa moja na hivyo kuwaongezea uzalishaji.
Mziray alimwagizwa Msofisa Ufuatiliaji wa TASAF Ilemela, Alex Kabona kusimamia kikunid hicho ili waandike maombi ya feha za nyongeza kiasi a Sh 2,500,000 na kuahidi kuwa fedha hizo zitatolewa na TASAF ndani ya majuma mawili.