Na Meleka Kulwa- Dodoma
Waziri wa zamani wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Mkurugenzi wa Timu ya JKT Tanzania Jemedari Said wamepitishwa kuwania ubunge kwenye Jimbo la Mtama katika mchakato wa ndani wa CCM.
Majina hayo yametangazwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla leo Jumanne, Julai 29, 2025, katika Ofisi za CCM jijini Dodoma
Wagombea wengine waliopita kwenye jimbo hilo ni Jabiri Mohamed Chilumba na Metta Cuthbert Nahonyo.