Na Meleka Kulwa – Dodoma
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza Majina ya wagombea walioteuliwa kugombea ubunge Arusha Mjini leo July 29,2025. Alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Chama hicho Jijini Dodoma
Majina Saba yamefanikiwa kurejea Paul Makonda, Ally Said , Hussein Gonga, Aminata Teule, Mustapha Nassoro, Ruhembo , Kishugua huku aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mrisho Gambo akiachwa.