Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, Ikulu ya Kigali, Rwanda.
Viongozi hao wameangazia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda pamoja na matunda ya
Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda, uliofanyika kwa siku tatu jijini Kigali, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Julai, 2025.